Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Je unaweza kucheza bila kukunja goti? Kama ndio, Mwana FA na AY wanakupa fursa ya kushiriki katika video ya hit song hiyo! Changamka

“Bila kukunja goti” ni moja kati ya hit songs za mwaka huu (2013) kutoka kwa maswahiba wawili wa muda mrefu Mwana FA na AY ambayo toka imetambulishwa zaidi ya wiki moja iliyopita imeanza kuonyesha dalili za kufanya vizuri.

FAAY

Kitu kimoja cha tofauti kuhusu wimbo huo waliomshirikisha Jay Martins kutoka Nigeria ni idea yake ya “kucheza bila kukunja goti”, kwanza mtu unapoisikia kwa mara ya kwanza lazima utatamani kujaribu walichokiimba kucheza bila kukunja goti sababu ni kitu ambacho sio cha kawaida.

Mwana FA na AY wameamua kuwashirikisha mashabiki wao ambao ndio walengwa wakubwa wa muziki wanaoufanya, kwa kuwapa nafasi ya kuwatumia vipande vya video walizojirekodi wakionesha staili zao tofauti za uchezaji bila kukunja goti, na wale watakaovutia kwa ubunifu watapata nafasi ya kushiriki katika video ya wimbo huo hivi karibuni.

Akiongea kupitia 255 ya XXL Hamis Mwinjuma aka Binamu amesema wale wote wanaopenda kushiriki katika video hiyo wanatakiwa kujirekodi wakicheza ‘bila kukunja goti’ na kisha ku upload vipande vya video zao youtube kwa kufuata maelekezo ambayo watayatoa baadaye.

Haya kama wewe ni mbunifu na shabiki wa Mwana FA na AY na ungependa kuonyesha uwezo wako wa kucheza ‘bila kukunja goti’ changamkia fursa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW