Michezo

Je ?, United wataweza kumshawishi mtukutu Paul Pogba kuongeza kandarasi, muda wa kusalia Old Trafford wahesabika 

Imeripotiwa kuwa Manchester United ipo katika mipango ya kumuongezea mkataba mpya kiungo wake Paul Pogba ili kuhakikisha anaendelea kusalia Old Trafford.

Image result for paul pogba in serously moment

Pogba mara kadhaa ameonyesha nia ya kutaka kuondoka United katika dirisha la usajili lililopita hasa kutua Real Madrid huku ikielezwa kuwa akihitaji changamoto mpya.

Ingawaje Madrid hawakuwahi kuweka mzigo mezani kwaajili ya Mfaransa huyo hali iliyo shuhudiwa United wakiendelea kuwa na nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 lakini  bado watu wanahusisha kutimka kwake kwa miamba hiyo ya Hispania.

Paul Pogba anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu lakini United  bado wanayo nafasi ya kuendelea na mazungo kwa miezi kadhaa.

Image result for paul pogba

Baadhi ya magazeti ya michezo nchini Uingereza yamedai kuwa Mashetani hao wekundu hawapo tayari kumuacha kiungo huyo kuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake hivyo wataendelea kumshawishi ili kuongeza kandarasi na kumuahidi kumuongezea dau nono katika malipo yake ya wiki.

Hata hivyo United itakabiliwa na vita kubwa ya kumshawishi mtukutu Paul Pogba kukubali kuongeza kandarasi huku kijana huyo akiwa anasimamiwa na wakala wake Mino Raiola na kaka yake Mathias Pogba.

Siku ya Jumanne kaka yake Pogba, Mathias alisikika akisema kuwa huitaji elimu kubwa kufahamu Zinedine Zidane anamuhitaji kiungo wa Manchester United.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents