Habari

Je Wajua? Mbu wamejifunza mbinu mpya ya kujikinga na chandarua chenye dawa

Jinsi ambavyo baadhi ya bakteria wasivyo na hofu siku hizi kuhusu antibiotics, ndivyo ambavyo mbu wamebuni njia mpya ya kujikinga na chandarua kilichowekwa dawa. Hii ni kutokana na utafiti mpya uliochapishwa na gazeti la ‘infectious Diseases”.

Utafiti huo uliofanywa kwa miaka minne katika nchi ya Papa New Guinea ili kuangalia ni kwa namna gani ugawaji wa vyandarua vyenye dawa vimeweza kusaidia kupiga vita ugonjwa hatari wa malaria.

Vyandarua vilivyopigwa dawa vimeonekana kama njia sahihi na yenye mafanikio kwenye kupunguza vifo zidi ya ugonjwa hatari wa malaria. Kutokana na takwimu zilizotolewa na American Council on Science and Health, kesi (case) tofauti tofauti milioni 451 zimeweza kuzuiwa za malaria katika miaka 15 iliyopita kutokana na utumiaji wa vyandarua vilivyowekwa dawa.

Utafiti huu umeonyesha kuwa mbu sasa hivi wamebadili utaratibu wa kuuma (feeding behavior) katika miaka ya hivi karibuni ili kujiepusha na vyandarua vyenye dawa.

Kabla ya ugawaji wa vyandarua vilivyowekwa dawa mbu walikuwa na tabia ya kung’ata kuanzia usiku wa manane. Lakini baada ya watu kuanza kutumia vyandarua vyenye dawa, mbu wamebadili ratiba yao ya kupata chakula na kuanza kung’ata kuanzia saa nne usiku (10 p.m) na wengine hung’ata kuanzia saa moja(7 p.m) mpaka saa tatu usiku (9 p.m). Ili kuwapata watu kabla hawajaingia ndani ya chandarua chenye dawa.

Kupungua kwa kesi (case) nyingi za malaria kutokana na kung’atwa na mbu kumefuatiwa na kuongezea tena kwa kesi hizo kiama ilivyokuwa awali kabla ya mgao wa vyandarua vilivyowekwa dawa kwa baadhi ya maeneo. Utafiti huo umekuwa unaleta matokeo tofauti tofauti pia katika vijiji tofauti tofauti.

Nitoe wito kwa watanzania tuendelee kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa kwani vimeonyesha kupunguza idadi kubwa ya kesi (case) za malaria, lakini pia tujitahidi kuweka mazingira safi yanayotuzunguka ili kufanya mazingira yetu yasiwe mazingira salama kwa mbu kuzaliana na kuishi. Malaria haikubariki, tuungane kutokomeza ugonjwa huu hatari wa malaria.

Your Health, My Concern

FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher/Pharmacist
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]
[email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents