Burudani ya Michezo Live

Je wajua ndege haziruhusiwi kupita juu ya makazi ya mchezaji bora duniani Lionel Messi kwa mujibu wa sheria za jiji la Barcelona ? / hii ndiyo sababu 

Hii haitokei dunia kote lakini fahamu kuwa fanya ufanyavyo kamwe huwezi kupita na ndege juu ya nyumba ya mchezaji bora kabisa duniani wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi.

 

Zipo baadhi ya sehemu duniani ndege kamwe haziruhusiwi kupita ambapo kwa kimombo wanaita ‘flight restriction zone’ na baadhi yake ni kama Washington, D.C. Mecca nchini Saud Arabia na baadhi ya maeneo nchini Malaysia.

Hivyo basi ndege kutoruhusiwa kupita kwenye anga hiyo kamwe hakuhusiani na uwepo wa mchezaji huyo maarufu duniani bali ni kutokana na sheria ambazo zimewekwa, ndege kutopita maeneo hayo ambayo ni Gava Mar, Viladecans na Castelldefels yaliopo karibu na fukwe za bahari ili kuepusha uchafuzi wa mazingira.

Image result for Castelldefels

Lionel Messi huishi kwenye halmasahauri ya Castelldefels jijini Barcelona nchini Hispania na ndege haziwezi kupita kwenye maene yake ni kutokana na sababu hizo za kimazingira kwa mujibu wa sheria za Barcelona.

Image result for You can't fly over Lionel Messi House

Eneo hili la Castelldefels hulindwa zaidi katika kuhakikisha linatunzwa mazingira yake kwakuwa lina uoto mwingi wa asili na hivyo kupelekea sheria za jiji la Barcelona kupiga marufuku ndege, kwasababu husababisha uchafuzi wa mazingira (Noise pollution) kwa viumbe hai wa porini wanaopatikana maeneo hayo.

Kwenye maeneo hayo ndege haziruhusiwi kabisa kupita pembezoni mwa fukwe za bahari mahala ambapo nyumba ya Messi pamoja na watu wengine maarufu wanaishi na sheria hiyo huwasaidia yeye na mastaa wengi mahala hapo kutobuguziwa na makelele ya ndege kupita angani ambapo ni kilomita 10 kufikia uwanja ulipo.

Kunapata umbali wa maili 12 kutoka Castelldefels hadi kufika kwenye uwanja wa Barcelona, Nou Camp huku wachezaji wengi wa timu hiyo wakiwa wamenunua nyumba zao za kuishi maeneo hayo.

Kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya watu hasa lilipokuja wazo la kutaka kuupanua uwanja wa ndege uliyo umbali wa kilomita 10  kutoka kwenye Manispaa hiyo na kushindikana wakati rais wa mashirika ya ndege Kimataifa ‘International Airlines Group (IAG),’ Javier Sanchez-Prieto aliposema ni karibu na makazi ya Messi.

Image result for You can't fly over Lionel Messi House

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW