Habari

Je wajua nini hufanya macho yaonekane mekundu ukipiga picha kwa kutumia kamera yenye flash?

Macho hutupa uwezo wa kuona vitu vinavyotuzunguka zaidi ya vile ambavyo panya na viumbe wengine wanavyoona na kujenga uwezo wao wa kufikiri.

Mwanga huingia ndani ya jicho kupitia cornea. Baada ya hapo mwanga hufanyiwa utambuzi na retina na taswira hupelekwa moja kwa moja kwenye ubongo kupitia optic nerve. Kiasi cha mwanga kinachoingia kwenye retina hudhibitiwa na pupil. Wakati wa mchana sababu kuna mwanga mkali, pupil husinyaa na kuruhusu mwanga kidogo kuingia ndani ya jicho.

Wakati wa giza, pupil hutanuka kuruhusu mwanga wa kutosha kuingia. Katikati ya retina na sclera (sehemu nyeupe ya jicho) kuna kiwambo chenye tishu zinazoitwa Choroid. Safu hii husambaza damu, virutubisho na oksijeni katika maeneno ya nje ya retina. Choroid ina mishipa mingi sana ya fahamu.

Mwanga wa flash ya camera unapotoka, pupil huwa haipati muda wa kutosha kusinyaa, hivyo basi kiasi kikubwa cha mwanga huakisiwa (reflected) na fundus (sehemu ya mbele ya jicho). Kutokana na choroid kuwa na mishipa mingi ya damu, hivyo basi mwanga unaochukuliwa na lensi ya kamera huonekana mwekundu. Mtu akiangalia picha yake ataona macho yake yanaonekana mekundu.

Kutokana na angle ambayo mwanga huingia kwenye jicho ni sawa na engo (angle) ambayo mwanga huakisiwa kutoka nje, na jinsi flash inavyokuwa karibu na lensi ya kamera ndivyo kunavyokuwa na uwezekano mkubwa wa mwanga ulioakisiwa kuonekana na lensi.

Sababu nyingine inawezekana kuwa ni kiasi cha melanin kwenye kiwambo nyuma ya retina na umri wa mtu anayepigwa picha. Watu weupe (light skinned people) wenye macho yenye rangi ya blue huwa wanakuwa na kiasi kidogo cha melanin kwenye fundus zao hivyo basi uwezekano wa macho yao kuonekana mekundu ni mkubwa kuliko watu weusi (dark skinned people) ambao wengi wao huwa na macho yenye rangi ya kahawia (brown).

Watoto wadogo pia wakipiga picha na kamera yenye flash kuna uwezekano mkubwa kwenye picha akaoneka ana macho mekundu, hii inatokana na ukweli kuwa pupils za macho ya watoto hutanuka kwa haraka kuliko za wakubwa hata kwenye mwanga mdogo sana.

FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher/Pharmacist
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents