Habari

Je, Waogopa Nini?

Sisi sote tunalo jambo tuliogopalo, ikiwa ni kitu kinachoonekana, au nl jambo la kijuujuu tu, lakini likianza kuvuka mipaka ya kiakili na kuingia katika woga usioeleweka, hapo huitwa “fobia”. Fobia, kufuatana na mabingwa wa masuala ya akili, ni woga wa kupita kiasi dhidi ya kitu au hali fulani.


Ninakiri kuwa yapo mambo ninayoyaogopa ambayo yanaweza kuhesabika kuwa hayaelaweki, kwa mfano woga wangu wa mijusi, jinsi watembeavyo, macho yao ya ushangam duh!! Ile hali ya kuandika habari zake tu inaufanya mwili usisimke.

Hata hivyo, tukiongea kwa utulivu, woga huu hakuna sababu ya maana ya kunifanya mimi nimuogope mjusi kwani hana madhara yoyote kwangu, na kwa upande mwingine akiwepo nyumbani, anasaidia kuwauwa wadudu kama mbu kama tulionao hapa Bongo!

Hata hivyo zipo fobia ambazo hazina maana na zinachekesha kweli, (lakini siyo kwa yule aliyenazo) na nyingine  zinastaajabisha sana. Kumbuka kuwa hizi ni fobia au woga wa kiukweli kama vile Bibliofobia-woga wa vitabu, kwa mtu ambaye ana woga huu, aonapo au agusapo vitabu, ataona kinya sawa na mimi nionapo mjusia tu. Hapa chini kuna orodha ya fobia ambazo tunadhani mtafurahia kuzifahamu pamoja na maoni yetu machche.

Ikiwa mnazifahamu nyingine, jisikieni huru kugawana nasi.

Androfobia – woga wa wanaume (itakuwaje kama wewe ni mwanume na unao woga huu?)
Afenfosmfobia – Woga wa kuguswa. (mtu huyu bila shaka huishi kwa kujitenga)
Barofobia – Woga wa mvuto wa graviti (bado sijaelewa woga huu ukoje na mtu mwenye kuwa nao afanyakazi vipi)
Bibliofobia – Woga wa vitabu. (huenda wale wanaohangaika shuleni wanao woga huu)
Cacofobia – Woga wa ubaya. (je, hii hutegemea juu ya mtazamo wa mtu kuhusu uzuri?)
Kromofobia – Woga wa rangi. (tena hapa, mtu anaishije katika ulimwengu uliojaa rangi?)
Kronomentrofobia – Woga wa saa.(Nadhani Waafrika wengi wana woga huu, lol)
Coulrofobia – Woga wa wachekeshaji au machale. (eti, wapo machale wengine niliowahi kuwaona, wanatisha kweli)
Gamofobia – Woga wa ndoa. (Yasikitisha kuwa wanaume wengi wanayo fobia hii)
Genufobia – Woga wa magoti. (Sijui magoti yao wanayafanyaje?)
Gynofobia – Woga wa wanawake (Wakati mwingine tunatisha)
Heliofobia – Woga wa jua (Vampaya au mumiani?)
Koinonifobia – Woga wa vyumba. (Ufumbuzi wa tatizo hili ni kuishi nje)
Leukofobia – Woga wa rangi nyeupe. Je hali hii inajumuisha hata watu weupe?)
Mageirocofobia – Woga wa kupika. (Nani yuko tayari twende kula nje?)
Melanofobia – Woga wa rangi nyeusi. (kwa hiyo mtu huyu anajenga ubaguzi wa rangi?)
Octofobia – Woga wa nambari 8. (Ndio nambari zinaweza kuwa athiri watu wengine)
Ornithofobia – Woga wa ndege. (Wapo ndege wanaotisha kweli)
Papyrofobia – Woga wa karatasi. Nimewahi kumuona mtu mwenye woga huu alidhani karatasi ni moto)
Filofobia – Woga wa upendo (kutoa au kupokea?)
Podofobia – Woga wa vikanyagio vya miguu. Hata mimi ninao woga huu lakini ikinuka tu!)
Porfyrofobia – Woga wa rangi zambarau. (filamu na maonesho ya  Broadway ya jina hilo mbona yalikuwa mazuri tu)
Scolionofobia – Woga wa shule. Nina wasiwasi na woga huu….)
Selenofobia – Woga wa mwezi. (hivo kinyume cha mumiani ni nini?)
Somnifobia – Woga wa usingizi. (pengine wamejijaza vidonge)
Teknofobia – Woga wa teknologia. (Kwa kawaida huwaathiri watu wa makamo)
Venustrafobia – Woga wa wanawake wazuri. (kama wewe unataka kuhakikisha kuwa wewe ni mzuri, mtafute mtu mwenye woga huu na tazama kama atakimbia)
Xenofobia – Woga wa wageni au watu usiowafahamu. (pia maarufu kama Skizoz)

Kwa nyingine tembelea hapa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents