Habari

Jeff Mnyamwezi Bye Bye Tanzania

Jeff MnyamweziKila mpenzi wa burudani ambaye ana kawaida ya kujimx viwanjani lazima atakuwa analijua jina la Jeff Mnyamwezi ambaye mara nyingi huoneakana akila bata ile mbaya na machizi mbali mbali wakiwemo…

Jeff Mnyamwezi


Kila mpenzi wa burudani ambaye ana kawaida ya kujimx viwanjani lazima atakuwa analijua jina la Jeff Mnyamwezi ambaye mara nyingi huoneakana akila bata ile mbaya na machizi mbali mbali wakiwemo wafanya biashara maarufu jijini na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, lakini mchizi hivi sasa yuko njiani kuelekea Afrika kusini baada ya kupata Passport yake ambayo ameisotea kwa takriban miaka 6 sasa.
{xtypo_quote_left}naenda Afrika kusini lakini najiona kama naenda Marekani – Jeff {/xtypo_quote_left}
Bongo5 ilipata bahati ya kukutana na Jeff Mnyamwezi akiwa katika harakati za kukusanya nauli kwa washkaji “mwanangu hivi unavyoniona ndio nimetoka kuchukua mkoba wangi sitaki hata kuchelewa kesho asubuhi nakamata zangu basi napotelea zangu kwa mkaburu nimeshachoka na maisha ya kuishi kwa kupiga mizinga sema nashukuru washkaji wamekuwa wakinisaidi bila kunichoka na hivi ndio nawazungukia kwa mara ya mwisho wanisaidie kwa mwenye chochote mi nitambae”


Mchizi hajui hata huko aendako anakwenda kufanya nini ila alichodai kuwa yuko na mwenyeji wake ambaye atampa maline yote mara watakapofika huko “ila nisikufiche mtu wangu mi naenda kazini sasa tuombeane tu nirudi salama, siwezi elezea jinsi ninavyojisikia kusafiri kwani nina paspoti sina nauli lakini kesho lazima nitambae kwani niko mbio ile mbaya kukichanga kwa masela, naenda Afrika kusini ila furaha niliyo nayo naona kama naenda Marekani usipime mtu wangu”


Jeff Mnyamwezi ana kipaji cha uchekeshaji kwani mara nyingi hutumia muda wake kuwafurahisha wale alio nao karibu na kujipatia rizki yake kwani washkaji huwa wanamtoa na mapene kiasi alimradi maisha ya mnyamwezi yanaenda…We Wish U all The Best Dawg.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents