Burudani

Jela yamuita tena Chris Brown

Chris Brown ameibua msala mpya ambao unaweza kumletea hatari kubwa ya kumpeleka jela.

Muimbaji huyo Jumatatu hii alihudhuria katika klabu ya usiku ya Aja Channelside iliyopo mjini Florida lakini alijikuta akiibua jambo jipya baada ya kumpiga ngumi mpiga picha mmoja aliyefahamika kama Bennie Vines aliyekuwa akipiga picha ukumbini hapo.

Imedaiwa kuwa wakati Chris alipokuwa katika klabu hiyo wainzi wake waliwakataza wapiga picha wote kumpiga picha msanii huyo huku uongozi wa klabu hiyo ya Aja Channelside ukidai picha zitapigwa na mpiga picha wao.

Lakini wakati Bennie akiendelea kuwapiga picha baadhi ya watu wengine alijikuta akiugulia maumivu asiyoyatarajia baada ya kuchapwa ngumi na Brown ambaye inadaiwa kuwa mpiga picha huyo alivunja masharti kwa kumpiga picha.

Hata hivyo inadaiwa Chris alitoweka eneo la tukio kabla ya polisi kufika. Tazama video ya tukio hilo hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents