Aisee DSTV!
SwahiliFix

Jenerali wa BongoFleva Australia ‘Simorix’ afunguka alivyojipanga (Video)

Msanii wa Bongo fleva Simorix the General Mtanzania anayeishi nchini Australia ameweka wazi kutangaza mziki wa huo nchini Australia kupitia mziki wake anaoufanya nchini humo.

Simorix alisema kuwa tayari ana nyimbo ambazo ameshazipika kilichobakia ni kuzisogeza kwa mashabiki zake ili waweze kuzipokea njimbo hizo.

“Nna kiu ya kupeperusha bendera yetu Australia kupitia mziki wa bongo fleva kwahiyo nina nyimbo kadhaa ambazo nitaziachia kabla ya mwaka haujaisha kikubwa ninaomba mashabiki waweze kuzipokea maana zote ni hit” alisema Simorix General.

Ameongeza Mipango ya hapo baadae ni pamoja na kuandaa matamasha na timu yangu kwa sasa akili kubwa nimeielekeza katika kutangaza kazi zangu nchini.

“kwa siku za baadae naweza kufikilia kuanzisha tamasha ila kwa sasa nguvu kubwa tunaiweka katika kupromote carrer yangu then nyimbo zetu zikijulikana na kupata supoti ndio tutaingia kwenye show rasmi”

Simorix The General mpaka sasa anatamba na kibao chake cha ‘tuna piga bao’ akiwa amefanya cover ya wimbo Shettah ‘Hatufanani’ huku beats ikiwa imetengenezwa na Kimambo na Director wa video ni Daniele Cernera kutokea Australia.Beat aliyotumia Simorix ndio beat iliyotumia mwanadada Nandy pamoja na Shetah.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW