BurudaniUncategorized

Jennifer Lopez achangia $1m wahanga wa kimbunga Puerto Rico

Jennifer Lopez ameamua kugawana alichokipata katika muziki na wahanga wa Puerto Rico.

Msanii huyo ameamua kuchangia kiasi cha dola milioni moja ambapo ni zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa fedha za kitanzania kwa wananchi hao waliopatwa na janga hilo la kukumbwa na kimbunga cha Maria siku chache zilizopita.

Akiongea katika mkutano wa kuchangia fedha hizo, uliofanyika Jumapili hii mbele ya Governor wa mji wa New York, Andrew Cuomo, Jennifer amesema, “Watu wa Puerto Rico ni wananchi wa Marekani na leo Puerto Rico inahitaji msaada wetu. Kimbunga cha Maria kimeharibu kisiwa chetu. Nakuomba ushirikiane na kuchangia kwa nguvu ya first lady wa Puerto Rico, Beatriz Rosselló.

“Pamoja, tunaweza kusaidia kukijenga tena kisiwa chetu na Caribbean,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents