Soka saa 24!

Jennifer Lopez avalishwa pete yenye thamani ya Dola mil 1 na mchumba wake, Ikiwa ni mara yake ya tano kuvalishwa pete ya uchumba na wanaume tofauti (+ Picha)

Wapenzi ambao wamekuwa kwenye mahusiano kwa takribani miaka miwili sasa, Mwanadada msanii wa muziki Jeniffer Lopez pamoja na mpenzi wake ambaye alikuwa mchezaji wa mchezo wa Baseball Alex Rodriguez wamevalishana pete tayari na pete hiyo ikikadriwa kuwa na thamani ya Dola milioni moja.

Mwanamuziki Jennifer Lopez mwenye miaka 49, amevishwa Pete ya Uchumba kwa mara ya 5 na wachumba wanne tofauti. Mara ya kwanza Jlo alichumbiwa mwaka 1997 na Ojani Nia penzi halikudumu sana baada ya mwaka wakaachana. 

Cris Judd aliyekuwa dansa wake kushika hatamu ndani ya mwaka mmoja tu penzi chaliii. Mwingine aliyewahi kulamba asali na pete akamvisha ni Muigizaji Ben Affleck couple iliyopewa jina Bennifer ndoa yao ilidumu kwa miaka miwili tu na kuvunjika. Baadae Jlo alichumbiwa na Muimbaji Marc Anthony na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili mapacha.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW