Habari

Jennifer Lopez kurejea katika meza ya ujaji wa American Idol msimu ujao?

Baada ya Nicki Minaj, Mariah Carey na Randy Jackson kuthibitisha kutoendelea na msimu ujao wa shindano la kusaka vipaji ‘American Idol’ msimu ujao, kuna dalili za Jeniffer Lopez kurejea katika meza ya ujaji wa shindano hilo mwakani.

Jennifer Lopez leaving her hotel in New York

Chanzo kimoja kimeiambia Peoples Magazine kuwa J Lo yuko katika hatua za mwisho za kusaini mkataba na American Idol kwaajili ya kuwa jaji katika msimu wa 13 wa shindano hilo linalotegemewa kufanyika mwakani.

J-Lo mwenye miaka 44 alikuwa jaji katika misimu miwili mfululizo kabla ya kujiengua mwaka jana kwasababu alihitaji kupata muda zaidi wa kufanya maswala yake ya muziki ikiwa ni pamoja na world tour.

Kwa mujibu wa Entertainment Weekly mastaa wengine ambao inasemekana kuna uwezekano mkubwa wakawa katika panel ya majaji wa Ameican Idol msimu ujao ni pamoja na Keith Urban, Jennifer Hudson na producer na mwimbaji wa Black Eyed Peas Will i.am.

Msimu wa 13 wa American Idol kwa sasa upo katika pre production na unategemewa kuzinduliwa January 2014.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents