Michezo

Jeraha la bega kumfanya Manny Pacquiao apumzike masumbwi kwa mwaka mzima

Manny Pacquiao ataweka gloves zake pembeni kwa mwaka mzima wakati akijiandaa kufanyiwa upasuaji kwenye bega lake na anaweza kukabiliwa na hatua za kinidhamu kwa kushindwa kuweka wazi jeraha hilo.

Manny

Bondia huyo wa Ufilipino alidundwa na Floyd Mayweather Jumamosi iliyopita kwenye pambano lao lililopewa jina ‘Fight of the Century’ lakini baadaye aliweka wazi kuwa aliumia bega lake wakati wa mazoezi japo ambalo analiunganisha na kushindwa kwake.

Pacquiao alikuwa akichomwa sindano za kupunguza maumivu wakati wa maandalizi lakini alikataliwa kuchomwa siku ya pambano hilo na tume ya wanamichezo ya jimbo la Nevada.

Jeraha hilo limesababisha kuwepo uwezekano wa mpambano wa marudiano kati yao mwezi September.

Ni jeraha lile lile kama alilolipa mchezaji wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant mapema mwaka huu na linaweza kuzusha wasiwasi kama Pacquiao ataweza kupigana tena.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents