Michezo

Jerome Valcke avuliwa madaraka rasmi Fifa

Katibu mkuu wa Shirikisho la soka duniani Fifa aliyekuwa amesimamishwa kazi Jerome Valcke ameondolewa rasmi kutoka kwenye wadhifa huo na shirikisho hilo.

160105203057_jerome_valcke_640x360_epa

Mfaransa huyo mwenye umri, 55, kwa sasa amesimamishwa kujihusisha na maswala yoyote ya kandanda baada ya kudaiwa kuhusika katika njama ya kufaidi kutokana na mauzo ya tiketi za Kombe la Dunia.

Fifa imependekeza apigwe marufuku kuhusika katika shughuli zozote za soka kwa miaka tisa.

Valcke, ambaye pia anakabiliwa na tuhuma za ufisadi, amekanusha madai hayo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents