Habari

Jeshi la polisi Dar latoa siku 7 majambazi kujisalimisha

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa siku saba kwa majambazi wote waliowahi kutumikia vifungo na kuachiwa kwa kumaliza vifungo au rufaa, wajisalimishe kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lucas Mkondya

Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Kamanda Lucas Mkondya mbele ya waandishi wa habari amesema lengo la kuwaita majambazi hao ni kutaka kupanga utaratibu mzuri ili waone kama baada ya vifungo vyao, wamebadilika na wanajihusisha na shughuli gani kwa sababu walikuwa ni majambazi sugu na walifanya matukio mbalimbali.

Kuanzia leo (jana) nataka wajisalimishe, wasipojisalimisha wanajua jinsi tunavyowatafuta kwa sababu ni jambazi hatumtafuti kwa kucheka tunamtafuta kwa silaha lengo la kuhakikisha hatusikii milio ya bunduki ikipigwa Dar es Salaam,”amesema Kamanda Mkondya.

Hata hivyo, Kamanda Mkondya amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa, kutoa taarifa kama kuna majambazi katika maeneo yao ambao wameachiwa ili polisi wawafuatilie kikamilifu.

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents