Habari

Jeshi la Polisi labaini watuhumiwa mauaji Kibiti

Jeshi la polisi nchini limetoa orodha ya majina 12 ya wanaotuhumiwa kuratibu na kuendesha harakati na mauaji ya viongozi wa serikali za vijiji katika wilayani Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.


Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Onesmo Lyanga

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amesema kupatikana kwa watuhumiwa hao pamoja na picha ni kutokana na oparesheni inayoendelea na vyombo vya ulinzi katika Wilaya hizo.

“Tumeweza kuwa baini Watuhumiwa wa mauaji hayo, Watuhumiwa hao wameweza kubainika kwa majina na picha kwa baadhi yao ni matokeo ya oparesheni inayoendeshwa na vyombo vya ulinzi, Mtuhumiwa wa kwanza ni Faraji Ismail Nangalava, Anaf Rashid kapera, Said Ngunde, Omary Abdalla Mandimbwa, Shaban kinyangulia, Haji Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Njame, Rashid Salum Mtulula, Shekhe Hassan Nasri Mzuzuzi, Hassan Uponda,” alisema Kamanda Lyanga.

“Jeshi la polisi limebaini haya kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi,” aliongeza.

Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kufichua kwa siri watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama katika mkoa huo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents