Shinda na SIM Account

Jeshi la Polisi lakamata abiria watatu waliokuwa wakigombania siti (+video)

Jeshi la Polisi mjini Hong Kong, nchini China limewashikilia abiria watatu waliokuwa wanazozana na kuvutana nywele kwenye treni la abiria wakigombania siti.

Abiria hao wakiwa kwenye mzozano wa kugombania siti.

Wanawake hao watatu wamekamatwa na polisi baada ya video yao kuvuja mtandaoni ikiwaonesha mmoja wao akivutwa nywele na kupigwa ngumi.

Polisi mjini Hongo Kong wamesema tukio hilo limetokea jana jumatano majira ya 12:00 asubuhi kwenye treni iliyokuwa inatoka Mei Foo kwenda Tuen Mun .

Kwa mujibu wa mtandao wa HK01.com wa nchini ambao ndiyo ulikuwa wa kwanza kusambaza video hiyo umeripoti kuwa tayari polisi wameshawatambua kwa majina watu hao kuwa ni Lau (54), Zhang (49) na msichana He mwenye miaka 24 wote walikamatwa katika kituo cha treni cha Tsuen Wan masaa machavhe baada ya tukio hilo.

Hata hivyo Polisi wamesema wanawashikilia kwa kosa la uvunjivu wa amani kwenye usafiri wa umma na wote afya zao zipo sawa isipokuwa Bi. Lau (54) aliyekuwa anavutwa nywele ndiye aliyepelekwa hospitali kwa matibabu.

Chanzo : Mtandao wa hk01.com

 

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW