Habari

Jeshi la Polisi lapiga marufuku ‘tinted’ kwenye kioo cha mbele ya gari

Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani limepiga marufuku uwekaji wa ‘tinted’ katika kioo cha mbele huku likiwataka wamiliki wote kuondoa mara moja kabla ya kuanza operesheni kwa watakaokaidi agizo hilo.

Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani, Mohamed Mpinga alipozungumza na Channel 10 na kusema uwekaji wa vioo vya tinted katika vioo vya mbele unawapa shida askari kutambua ni nani aliyepo katika gari husika kwa haraka huku akisema huchangia matukio ya uhalifu.

“Mimi tu niseme kuanzia sasa napiga marufuku wale wote walioweka tinted kwenye magari yao vioo vya mbele watoe mara moja, na sisi tutachukua hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaokuwa wameweka tinted kwenye vioo vya mbele, hata pembeni hatuwezi sema lolote lakini naweza sema kwamba anaeweka tinted kioo cha mbele anaficha nini? alihoji,alisema Kamanda Mpinga huku akihoji.

“Ikumbukwe kwamba sasa hivi yapo matukio kadhaa yanayotokea katika nchi yetu na kama unaweka tinted kwenye kioo cha mbele hivi unaficha nini?.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents