Habari

Jeshi la polisi latoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao

Msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania, Barnabas Mwakalukwa amewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kuchangia taarifa zenye mwelekeo wa kichochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwakalukwa Mwakalukwa amesema taarifa zinazoenea mitandaoni pamoja na picha za askari wa Jeshi hilo kuonekana Nairobi nchini Kenya kuwa anafuatilia taarifa za Tundu Lissu si za kweli na hazina ukweli wowote.

“Mmeelezwa kuwa kachero huiyo alionekana Nairobi jeshi la polisi lina kanusha taarifa hizo ni za uongo ni za kizushi tena ikumbukwe kwamba jeshi la polisi linafanya kazi kwa kutumia utawala wa kisheria na kwa huyo askari ni kweli alikuwa pale Nairobi kwa mafunzo kuanzia tarehe 4 mwezi wa 9, 2017 na akarejea nchini Tanzania tarehe 8 mwezi 9 mwaka 2017 na anaendelea kufanya kazi zake hapa,” alisema Mwakalukwa.

“Jeshi la polisi tunashangaa watu wanataka kujiletea umaarufu kwa lengo la kuchafua jeshi la polisi na serikali lakini pia kwamba kitu ambacho kinaonekana wazi tukio limetokea tarehe 7 askari wetu yupo kule kuanzia tarehe 4 na amerudi tarehe 8 inakuaje ahusishwe kwenye mambo kama hayo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents