Habari

Jeshi la Polisi latoa onyo msimu wa sikukuu

Jeshi la polisi nchini limetoa onyo kali kwa wananchi waliojipanga kufanya uhalifu katika kipindi cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akiongea na waandashi wa habari jijini Dar es salaam, Msemaji wa jeshi hilo Mratibu Mwandamizi, Advera Bulimba amesema kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia nafasi hizo kwa ajili ya kufanya uhalifu ikiwa ni pamoja na wale wanaojipatia kipato kisicho halali.

Aidha Bulimba alisema kuwa, “Jeshi la polisi tumejipanga vyema na hatutaruhusu mtu yeyote aharibu amani ya nchi kwa sababu zake binafsi, tunaomba wananchi watoe ushirikiano wa kutosha katika kushiriki ulinzi shirikishi.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents