Habari

Jeshi la Polisi mkoani Arusha laua majambazi watano baada ya majibizano ya risasi yaliyochukua takribani dakika 35 – Video

Jeshi la Polisi mkoani Arusha laua majambazi watano baada ya majibizano ya risasi yaliyochukua takribani dakika 35 - Video

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuua majambazi sugu watano, wakati wa majibizano ya risasi na polisi tukio lilitokea usiku wa kuamkia leo Januari 30, 2020,maeneo ya njia panda ya Matevez, Kata ya Olmot.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,ACP Jonathan Shanna.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Jonathan Shanna, na kusema kuwa majambazi hao walipanga kwenda kufanya tukio la ujambazi katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, na ndipo polisi walipopewa taarifa hizo na wao wakaweka mtego.

“Majibishano hayo yalichukua dakika 35, ambapo majambazi wanne walifariki papo hapo na mwingine aliyegeuza pikipiki yake na kukimbia umbali wa mita 500, na yeye alipigwa risasi na kudondoka, na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru” amesema Kamanda Shanna.

Aidha ACP Shanna amevitaja vifaa mbalimbali vilivyokutwa eneo la tukio, kuwa ni pamoja na Pikipiki 3, bunduki moja aina ya shortgun pump action, Chinese Pistol 1 iliyofutwa namba zake za usajili, Magazine 2 za Chinese, maganda 7 ya risasi za Chinese Pistol , risasi 2 za bunduki ya shortgun, maganda 5 ya risasi ya shortgun pamoja na simu mbili.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents