Michezo

Jeshi la soka Morocco kutua Dar

 

Timu ya taifa ya Morocco inatarajiwa kuwasili nchini oktoba 8 tayari kwa mchezo wa awali wa kombe la mataifa ya Afrika 2012 dhidi ya Taifa stars.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana B5, shirikisho la soka Morocco (FRMF), kikosi hicho kitatua nchini kikiwa na wachezaji 22 akiwemo Marouane Chamarh wa timu ya Arsenal.

Wengine wanaotarajiwa kuwasili nchini siku hiyo ni makipa Karim Fegrouch,Nader Lamyaghri,na Ahmed Mouhhamadina wa Oiympique Khouribga pamoja na mabeki Mehdi Benatia, Adil Karrouchy, Fettah Boukhhris, Morad Ally Rachid Soulainmani, Michael Chretian Basser, Chakib Benzoukane na Hicham Mohdoufi.

Viungo ni Adil Hermach, Mohamed Berabeh, Issam Errak, M’bari Boussoufa, Karim Al Ahmadi na Nabil El Zhar, ambaye anachezea klabu ya Liverpool ya England.

Washambulijini ni Mouniir El Hamadaoui,Chamakh,Youssef El Arabi,Adil Taarabt na Youssef Hadji.

Kocha wa timu hiyo Mfaransa Dominique Cuperly amejigamba kuwa ataibuka na ushindi siku hiyo katika mechi itakayochezwa katika uwanja wa Taifa jiji Dar

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents