Tupo Nawe

Jeshi la Sudan kutoa tamko muhimu muda wowote kuanzia sasa, nyimbo za mapinduzi zaendelea kuimbwa

Luninga ya taifa ya Sudan imesema jeshi la nchi hiyo linatarajiwa kutoa ‘tamko muhimu’ muda wowote kuanzia sasa baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya wananchi kutaka Rais Omar Al Bashir kuachia ngazi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Aljazeera msomaji habari wa luninga ya taifa amesema “Jeshi la Sudan linatarajia kutoa tamko muhimu muda wowote kuanzia sasa, hivyo kukaa na kusubiri,” amesema msoma habari huyo.

Maandamano hayo yaliyoanza kutokea mwezi Desemba, yamezidi kuwa changamoto kubwa kwa utawala wa Rais utawala wa Bashir.

Hadi Alhamisi hii inakuwa siku ya sita kwa waandamanaji hao kuwa nje ya makao makuu ya jeshi ambapo pia kuna nyumba ya Rais Bashir na ofisi za wira ya ulinzi.

Makundi ya waandamanaji wamekuwa wakilala mahala hapo huku wakiimba nyimbo mbalimbali za mapinduzi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW