Habari

Jeshi la Sudan limesaini makubaliano ya kugawana uongozi na upinzani, waweka makubaliano haya

Jeshi la Sudan limesaini makubaliano ya kugawana uongozi na upinzani, Makubaliano hayo yanatazamia miaka mitatu ya uongozi wa pamoja utakaofuatwa kwa uchaguzi mkuu

Jeshi la Sudan limesaini makubaliano ya kugawana uongozi na upinzani. Baraza tawala la kijeshi na viongozi wa upinzani nchini Sudan, wamesaini makubaliano ya kugawanya uongozi baada ya mazungumzo ya usiku kucha kumaliza mzozo nchini humo. Kumefanyika sherehe zilizomalizika hivi punde katika hoteli ya Corinthia katika mji mkuu wa Khartoum.

Kwa mujibu wa BBC. Makubaliano hayo yanatazamia miaka mitatu ya uongozi wa pamoja utakaofuatwa kwa uchaguzi mkuu.

Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, viongozi wa pande zote wamezungumzia kizazi kipya katika taifa ambalo limeshuhudia ghasia na maujai ya mamia ya waandamanaji tangu kutimuliwa kwa kiongozi aliyekuwepo Omar El Bashir mnamo April.

Tutakuarifu zaidi kadri tunavyoendelea kuipokea taarifa hii.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents