Habari

Jeshi la SUDAN limeshikilia makao makuu ya waasi jijini KHARTOUM

Jeshi la Sudan limefanikiwa kuyashikilia Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama wa Taifa cha nchi hiyo, ambacho kilikuwa kinamuunga mkono Rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir.

Askari kutoka kitengo cha Usalama wa Taifa walisambaza video zinazowaonyesha wakifyatua Risasi Hewani kama Alama ya Uasi na kuonesha nguvu zao. Kitengo cha Usalama wa Taifa kimevunjwa kwa sasa

Kiongozi Mwandamizi wa Baraza huru ambalo linaongoza Sudan hivi sasa, Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo ameshutumu Salah Gosh ambaye ni Mkuu wa Zamani wa Usalama wa Taifa kwa uasi huo na kusema jambo hilo sio la kuvumilia. Hata hivyo, amesema hachukulii jaribio hilo kama jaribio la mapinduzi

Hivi sasa kuna mabadiliko mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini Sudan na kumekuwa na wasiwasi kuwa baadhi ya viongozi waliokuwa na nguvu kipindi cha utawala wa al-Bashir watajaribu kuwekewa vikwazo kwenye harakati hizo

Desemba mwaka jana, al-Bashir alishtakiwa kwa tuhuma za rushwa na alihukumiwa kifungo cha miaka miwili katika Kituo cha Kijamii.

By Enjo Mmasi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents