Habari

Jeshi laahirisha mkutano kuhusu kukabidhi madaraka kwa raia, Mali

Watawala wa kijeshi nchini Mali wameahirisha mkutano wao wa kwanza uliohusu mpango wa kurejesha madaraka kwa raia baada ya kuongezeka kwa mvutano miongoni mwa viongozi wakuu ambao walisababisha mapinduzi ya Agosti 18.

Mali junta postpones first meeting over transfer of powers – Bioreports

Wanajeshi waliyaalika makundi ya asasi za kiraia, vyama vya siasa na waasi wa zamani kwa lengo la kufanikisha mashauriano.

Lakini taarifa ya watawala hao wa kijeshi ilieleza kwamba mkutano umeahirishwa katika dakika za mwisho hapo jana hadi utakapotajwa tena kutokana na kile walichosema “sababu za kimaandalizi”.

Kundi la muungano wa waandamanaji ambalo lilikuwa likifanya maandamano dhidi ya Rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keita, linalojulikana kama “June 5 Movement” halikualikwa kushiriki mkutano huo.

Kundi hilo linataka utawala wa kijeshi kuwajibika katika kufanikisha utawala wa kiraia kama ulivyoahidi, pamoja na kutoainishwa muda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents