DStv Inogilee!

Jibu la Lady Jaydee kuhusu kufunga ndoa na Spicy

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Lady Jaydee amesema suala la yeye kufunga ndoa na mpenzi wake Spicy watu waliache kama lilivyo kwani ni ishu ya maisha binafsi zaidi.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘I Miss You’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa watu kutokuwa na haraka na suala hilo na haelewi ni kwanini amekuwa akiulizwa kila mara.

“Kwanini watu wanapenda sana kupangia watu maisha, mgekuwa mnaacha vitu vinaflow , mtu kamaliza shule unanza kumuambia mbona hufanyi kazi wakati mtu labda ameomba kazi hajapata, unaulizwa mara unaolewa lini, unaulizwa unazaa lini waache watu waishi maisha yao, msitengemee vitu sana” amesema Lady Jaydee.

“Watu walishakula ubwabwa na mambo yakashindikana vile vile, sasa husilazimishe kama mtu hajajiandaa kwanini mtake kulazimisha ubwabwa?. Wanapenda kumpangia mtu kitu afanye wakati hataenda kuishi naye mwisho wa siku mkumbuke haya ni maisha yangu, kwa hiyo nadhani tungeyaacha tukajikita kwenye muziki tu” amesisitiza.

Lady Jaydee amekuwa katika mahusiano na msanii mwenzake Spicy kutoka nchini Nigeria, pia wameweza kutoa ngoma pamoja ambayo remix ya ngoma ‘Together’ ambayo hapo awali ilifanyika na Spicy pekee.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW