Jibu la Lava Lava kuhusu kufanya cover ya ngoma ya Alikiba

Msanii wa muziki Bongo, Lava Lava amefunguka iwapo anaweza kufanya cover ya ngoma yoyote ya msanii Alikiba.

Muimbaji huyo kutoka label ya WCB ameiambia The Playlist ya Times Fm kwa sasa bado hajafikiria hilo ila Alikiba ni msanii ambaye anajifunza mengi mazuri kutoka kwake.

“Kwa sasa hivi siwezi kusema, unajua mpaka kufanya cover ya msanii inabidi huo wimbo uwe unaufuatilia, unajua kufanya cover ni ku-present kile ambacho amekifanya lakini kukiboresha zaidi,” amesema.

Utakumbuka Lala Lava alishafanya cover ya ngoma ya Diamond inayokwenda kwa jina la Utanipenda.

Alipoulizwa ni kitu gani anajifunza kutoka kwa Alikiba alijibu; “vitu vingi sana, Alikiba ni msanii mzuri na anafanya vizuri, kwa hiyo wasanii wote wanaofanya vizuri lazima uchungulie kuona wanafanya vitu gani ili ujifunze,”.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW