Burudani

Jibu la Nikki wa Pili iwapo Joh Makini atakuja na bidhaa za kondomu

Rapper wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amezungumzia taarifa za Joh Makini kuja na bidhaa za kondomu.

Nikki ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kihasa’ amesema kuhusu ujio wa bidhaa hizo bado mazungumzo yanaendelea ila kitu ambacho kipo.

“Ile ni biashara ya Joh Makini sitaki kuizungumzia ila nachoweza kusema ni kwamba kuna watu ambao wapo, wapo katika mambo ya testing,” Nikki ameiambia Bongo5.

“Wakifanikiwa na kukidhi vigezo vyote Joh Makini atakuja public, bidhaa zake zitakuja public lakini kwa sasa wapo kwenye meza wanafanya kazi,” ameongeza.

Iwapo dili hilo litafanikiwa Joh Makini ataungana na wasanii Bongo Flava kama Diamond, Jux, Shetta na wengineo kutangaza bidhaa zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents