Jibu la Rayvanny iwapo Rich Mavoko ameondoka WCB

Msanii wa muziki Bongo kutokea WCB, Rayvanny amefunguka kuhusu taarifa zinazodai kuwa Rich Mavoko hayupo tena katika label hiyo.

Muimbaji huyo amesema ingawa yeye si msemaji rasmi wa suala hilo ila Rich Mavoko bado yupo nao WCB na wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara.

Taarifa za Rich Mavoko kutokwepo WCB zilianza kuchipuka June 19 , 2018 baada ya muimbaji huyo kutoonekana katika mkutano na waandishi wa habari ambapo Diamond alizungumza na wasanii wote wa WCB walikuwepo. Hata hiyo Babu Tale alieleza kuwa siku hiyo Rich Mavoko alikuwa aki-shoot video ya wimbo wake.

“Ujue sisi tunachekiwa kwenye group, leo kuna tukio hili na hili, so ukiona huyo kakosa ni masuala ya uongozi sana labda angekuwepo Diamond au Babu Tale angeweza kuongea sana lakini Mavoko yupo Wasafi kila siku,” amesema.

“Anakuja, anajiunga kwenye vitu lakini yeye kutokuja siku ile sijui sababu, kama kuna vitu vinavyoendelea ni yeye na uongozi. Mimi siwezi kuongea sana kwa sababu Mavoko ni mwanangu tunaongea tunachati, tunarekodi ngoma zetu,” Rayvanny ameiambia Wasafi TV.

Rich Mavoko alijiunga WCB mwaka 2016 akiwa kama msanii wa tatu kusaini baada ya Harmonize na Rayvanny, wimbo wake wa kwanza kutoa chini ya label hiyo unakwenda kwa jina la Ibaki Stori. Akiwa WCB ameweza kufanya kolabo na Harmonize na Diamond pamoja na kushiriki katika wimbo ‘Zilipendwa’ ambao uliwakutanisha wasanii wote wa label hiyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW