Burudani

Jibu la Rayvanny kwanini kolabo na Jason Derulo haijatoka

Msanii wa muziki Bongo, Rayvanny amefunguka kinachokwamisha kolabo yake na Rayvanny kutoka.

Muimbaji huyo wa WCB ambaye June 26 mwaka huu alionekana studio na Jason Derulo ameiambia The Base, ITV kuwa kazi hiyo ilishafanyika ile anasubiri Derulo aimalizee mixing kisha amtumie.

“Nilifanya ngoma kwenye studio yake lakini ratiba yake inakuwa imebana sana anakuwa anazunguka kwenye miji mingi tofauti, so akaniambia siwezi nikakutumia kitu ambacho hakijakaa proper subiri mpaka tuimix vizuri” amesema Rayvanny.

Hata hivyo Rayvanny ameeleza kuwa katika safari yake ya sasa ya Marekani ambapo ameenda kwa ajili ya ku-shoot video atafuatilia na hilo pia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents