Burudani

Jidenna aikutanisha Marekani na Afrika kwenye EP yake mpya

Jidenna ameachia EP yake mpya kwa kushtukiza iitwayo ‘Boomerang’.

EP hiyo ina ngoma tano ndani yake ikiwemo Decibels, Boomerang, Spy Candy, Bambi Too na Little Bit More.

Msanii huyo wa Marekani ambaye pia ana asili ya nchini Nigeria, amefanya hivyo ikiwa ni miezi tisa imepita tangu alipoachia albamu yake mpya iitwayo ‘The Chief’.

Katika EP hiyo Jidenna amewashirikisha wasanii wa Marekani na wengine kutoka Afrika akiwemo Quavo, Tiwa Savage, Malek Berry, Sarkodie na Burna Boy. Kwa sasa EP hiyo imeanza kuuzwa kupitia mtandao wa Apple Music.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents