Burudani

Jikubali: Single mpya ya Ben Pol inayokutaka kujithamini na kufuata ndoto zako (isikilize hapa)

Katika point fulani za maisha kila mtu huhitaji kupewa moyo, kuwa motivated, kupongezwa na kukumbushwa. Single mpya ya Ben Pol, Jikubali, itaishi kwa muda mrefu kwakuwa kwa namna nyingi itarelate na maisha ya watu wa kila rika kwakuwa kila mwanadamu huwa na mtu wa kumwangalia (role model).

Katika Jikubali, Ben Pol anawapa moyo vijana kujikubali, kufanya kazi kwa bidii, kujiamini na kutoziacha ndoto zao. Ni wimbo mzuri ambao unaweza kubadilisha maisha ya wengi.

Haya ni mashairi yake.

Verse1;

Unaweza kuwa Doctor, unaweza kuwa Star
Unataka kuwa Linah, unaweza kuwa Shaa
Kipaji Mali yako, Elimu Ngao yako
Usiache jambo Kati kwenye maisha yako
Unaweza kuwa Diamond, unaweza kuwa Jay
Unaweza kuwa JB, unaweza kuwa Ray
Mi Nakuasa it’s your time,
Huwezi kuwa chini you’ve got somethin’ special
Unampenda Lady Jay dee unamzimia Zitto
Trust me iko siku utatimiza ndoto yako
You can be a Boss, you can be a Lawyer
You can be the President
You’ll be successful

Chorus;
Wakati wako ndio leo (leo)
Kutimiza malengo yako,
Nakusihi Anza sasa (sasa)
Jishughulishe utapata (rudia mara mbili)

Verse 2;

Utavunja vunja miamba, hamisha milima
Vikwazo lazima nawe usirudi nyuma
You’ll be a hero, you can be the best
You can be a leader (dedicate yourself)
Tanzania ni yako, penda watu wako
Kuwa mfano bora kwenye jamii yako
Star Kama AY , kufika alipo FA
Inawezekana if you work hard in it
Na utafika mbali utazame ulikotoka
Mbunifu mwenye hadhi kama Hadija Mwanamboka
Unaweza kuwa rubani, unaweza Hakimu
Unataka kuwa Salama, unaweza kuwa Hasheem’

(Rudia chorus)

(Bridge)
You can be a champion (Jikubali)
You can be a teacher (Jikubali)
You can be a leader (Jikubali)
You can be a Preacher (Jikubali)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents