Burudani

Jikubali ya Ben Pol ni zaidi ya wimbo, ni kampeni ya kuhamasisha vijana, video kutoka June 1

Msanii mwenye nominations 5 katika KTMA 2013, Ben Pol anatarajia kuachia video ya single yake mpya ya Jikubali aliyoshoot jijini Arusha na mwongozaji Nisher. Mkali huyo wa RNB Tanzania ameelezea sababu za kuchelewa kuiachia video hiyo kuwa aliamua kuipa muda kidogo audio ili watu waielewe zaidi kabla ya kupata video.

ben2

Jikubali ya Ben Pol imeenda mbali zaidi ya kuwa single mpya tu ya Ben Pol sababu ameamua kuifanya kuwa kampeni ya kuhamasisha vijana mbalimbali hasa wanafunzi kutumia fursa walizonazo za kusoma hususani katika kipindi hiki ambacho matokeo ya kidato cha 4 yamekuwa hayaridhishi.

Akizungumza na Bongo5 amesema, June 15 anatarajia kufanya tamasha la bure katika viwanja vya Mnazi mmoja ambalo litakuwa ni kwaajili ya watu wote hasa wanafunzi ambao watapatiwa hamasa na watu mbali mbali akiwemo Ben Pol mwenyewe, wanasaikolojia na watu wa fani mbalimbali kama njia ya kumpa moyo kijana na kumhamasisha asikate tamaa katika ndoto alizonazo. Katika Tamasha hilo kutakuwa pia na performance ya wasanii mbalimbali akiwemo yeye mwenyewe.

Upande mwingine Ben amesema pamoja na kwamba single yake ya ‘Jikubali’ imepokelewa vizuri lakini amepokea changamoto kutoka kwa baadhi ya watu ambao wamemletea nyimbo kama 4 za nje ambazo zinafanana na Jikubali kwa maana ya ‘copy’. “Haziniletei changamoto sana sababu mimi niliconcentrate kwenye message zaidi ila flow ya uimbaji nilipanga iwe rahisi zaidi ili isimsumbue mtu wa kawaida kabisa”, alisema Ben Pol.

Ben wakati anaiachia Jikubali aliwahi kusema wimbo wa kundi la The Script ‘Hole of Fame’ ndio ilim-inspire kuandika ‘Jikubali’.

Nyimbo zingine ambazo zimefanana na Jikubali alizokuja kuletewa na watu tofauti ni pamoja na Miguel – Sure Thing na Lupe Fiasco na Guy Sebastian – Battle Scurs.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents