Burudani

Jina la mtoto wa Kanye West na Kim Kardashian lafahamika, anaitwa……..!

Wengi walitarajia kuwa mtoto wa Kanye West na Kim Kardashian aliyezaliwa (June 15) huenda angepewa jina linaloanzia na herufi ‘K’ kama ulivyo utamaduni wa familia ya Kardashians, well! Speculations hizo zilikuwa zimeelekea ‘KUSINI’ wakati ukweli umekuja kutokea ‘KASKAZINI’, utanielewa sasa hivi tu.

North parents

Kwa mujibu wa TMZ mtoto huyo wa kike wa mastaa hao amepewa jina la mwelekeo, yaani namaanisha kama jina la pili la baba yake ni Magharibi ‘West’ sasa yeye anaitwa Kaskazini ‘NORTH’.
Naomba nimtambulishe vizuri, mtoto wa kike wa Kanye West na Kim Kardashian amepewa jina la ‘NORTH WEST’ kwa mujibu wa birth certificate kutoka Cedars-Sinai hospital.

Lakini chanzo kingine kilichokaribu kimeuambia mtandao wa USWeekly kuwa couple hao tayari wamempatia mwanao nickname, atakuwa anaitwa ‘NORI’ kama kifupi cha North.

So Kim mwenye miaka 32 amepata a.k.a nyingine ambayo ni mama ‘North’ au mama ‘Nori’. Haijajulikana bado sababu za Kanye na Kim kuchagua jina la North.

Wewe unalionaje jina la mtoto huyo?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents