Habari

Jina la mtoto wa Prince William na Kate wa Uingereza lafahamika

Baada ya mtoto wa kifalme kuzaliwa Jumatatu wiki hii katika familia ya kifalme ya Prince William na Kate wa Uingereza hatimaye jina la mtoto huyo lawekwa wazi.

prince george

Mfalme huyo wa baadaye amepewa jina la GEORGE ALEXANDER LOUIS. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Daily Mail mtoto huyo atakapofikia hatua ya kutawala ataikwa King George VII, na kabla ya hapo atakuwa akifahamika kama Prince George.

william n kate

Uamuzi wa jina la mtoto huyo umefanywa jana na wazazi wake William na Kate ikiwa ni siku mbili tu toka azaliwe, tofauti na wakati baba yake William anazaliwa (1982) ambaye jina lake liliwekwa wazi baada ya siku saba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents