Burudani

‘Jinamizi’ lazidi kuwaandama Blac Chyna na Rob Kardashian kupitia Dream

Bado jinamizi lina waandama Blac Chyna na Rob Kardashian, ambao waliwahi kuwa katika mahaba mazito yaliyopelekea kupata mtoto mmoja aitwaye Dream.

Rob na Chyna kwa sasa ni kama chui na paka, pia linapokuja swala la  malezi ya mtoto wawili hao wanaingia  katika mgogoro upya, kwani baba wa mtoto huyo amekuwaa akidai kuwa Chyna hawezi kumlea mtoto kutokana na utumiaji madawa ya kulevya hivyo ana hatarisha usalama wa mtoto huyo.

Kufuatia hali hiyo Mahakama moja jijini Los Angles inayoshughulika na maswala ya watoto na familia imeanza kupata wasiwasi juu ya maisha ya mtoto huyo, hivyo jaji wa mahakama hiyo ameamuru kufanyika uchunguzi wa haraka  juu ya madai yanayomuhusu Chyna kutumia madawa ya kulevya kuji hakikishia kama kuna usalama kwa Dream.

Rob na Chyna wameingia katika ugomvi mzito uliowahi kupelekea akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram wa kijana huyo kutoka familia ya Kardashian kufutwa baada ya kuposti picha za utupu za mzazi mwenzake, ambapo alimtuhumu kumsaliti mara kadhaa kwa kuwa na wanaume wengine na pia amekuwa akidai kuwa Chyna anatumia wa madawa ya kulevya, kitendo ambacho amekuwa akipinga vikali mrembo huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents