DStv Inogilee!

Jinsi mnaijeria, Alex Okosi alivyoishawishi MTV kuanzisha MTV Base Africa

Mzaliwa wa Nigeria Alex Okosi ni rais na mkurugenzi mtendaji wa MTV Networks Africa.
Takriban miaka saba iliyopita aliwashawishi mabosi wake wa MTV kuanzisha tawi la kituo hicho barani Afrika la MTV Base katika kipindi ambacho hakukuwa na fursa katika bara la Africa.

Mwaka 2005, Africa haikuwa ikipendeza kwenye vyombo vya habari kama ilivyo leo. Habari nyingi kuhusu Afrika zilikuwa zikihusu umaskini, vita na maradhi.

Hata hivyo kutokana na kuzaliwa na kukulia nchini Nigeria, Alex Okosi alijua na aliamini fursa ya kipekee katika bara la Afrika ambazo zingeweza kuwa mchango mkubwa kwa kampuni ya MTV.

Katika kipindi cha African Voices cha CNN kinachoendeshwa na Nkepile Mabuse, Okosi alisema baada ya kuwakilisha wazo lake kwa mabosi, aliambiwa kuandaa mpango wa biashara ambao ungetumika kama uthibitisho kuwa Afrika ni soko nono kwa kituo hicho bingwa kwa burudani duniani.

Hiyo haikuwa kazi rahisi. Kipindi hicho, nchi kama Nigeria ilikuwa haina kabisa data za soko la matangazo. Pasipo kukata tamaa, Okosi ilibidi atumie mtandao wa marafiki wa marafiki wa marafiki pamoja na ndugu waliomsaidia na kumkusanyia data zilizokuwa hazipatikani kuhusiana na soko la matangazo.

Alex Okosi, receiving the award for New Champions for an Enduring Culture

Kidogo kidogo, alipata wazo ambalo liliuvutia uongozi wa MTV Networks na hatimaye kupewa ruhusa ya kuendesha biashara hiyo kwa kupewa cheo cha makamu wa rais na mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho barani Afrika.

Okosi akapewa jukumu la kuianzisha MTV Base katika kipindi hicho video za muziki wa Afrika hazikuwa na viwango vya kuridhisha. Kwa mujibu wake kipindi hicho, ubora wa nyimbo zilizokuwa zikifanyika barani Afrika haukuwa mzuri kama zinazopatikana kwa sasa lakini pamoja na hivyo aliamua kujikita kutafuta ubora.

Alisema ilimlazimu pia kufanya semina na mafunzo kwa maproducer na waongozaji wa video barani Afrika yaliyotolewa na wataalam wa kimataifa wa masuala hayo kuwapa ujuzi zaidi.

Ili kupata watazamaji wengi, ilimlazimu kutafuta ushirikiano na vituo vya runinga vya nchi mbalimbali ili kuionesha brand ya MTV Base kwa mamilioni ya watazamaji wa barani Afrika ambao hawakuwa na uwezo wa kununua madishi ama runinga za cable.

Mwaka 2008, alianzisha MTV Africa Awards ambazo zilisaidia kuongeza umaarufu wa wasanii wa Afrika ndani na kimataifa.

Kuiweka MTV Base kwenye ramani ya vituo vya runinga vinavyoheshimika barani Afrika halikuwa jambo rahisi lakini aliamua kukomaa na lengo lake ya kupromote vijana wa Afrika na utamaduni wa pop.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW