Habari

Jinsi teknolojia inavyoua mahusiano ya watu mbalimbali

Nilikuwa nikisoma makala moja iliyoandikwa wakati wa siku ya wapendanao, inazungumzia mpenzi mmoja wa kiume alipotengeneza picha kama zawadi ya kuweka kwenye meza ya mpenzi wake inayosema ‘mpenzi wangu ninakupenda sana kuliko simu yangu.’  

couple-staring-at-their-phones

Hii ndio makala yetu ya leo! Sio kawaida lakini inatokea kwamba kuna baadhi ya watu wanahisi mahusiano yao yanapambanishwa na teknolojia hivyo hawajui kama wanapendwa wao tena au simu za kisasa zinapendwa zaidi na wapenzi wao kuliko wao wenyewe kupendwa.

Teknolojia ni kitu cha kushangaza sana, inaruhusu wewe kuwasiliana na watu walio mbali kana kwamba wapo karibu na wakati mwingine unajikuta unatengeneza marafiki ambao hujawahi hata kuonana nao na vile vile ukaweza kuendesha biashara kutoka sehemu yoyote duniani bila kufungwa na mipaka. Hivyo huwezi kukataa kwamba teknolojia imeleta fursa za kutosha na imeweza kuboresha huduma nyingi sana kuliko hapo zamani.

Kutokana na faida nyingi vile vile teknolojia imekuja na mabaya yake na kama tukishindwa kuyatambua na kutowajibika namna tunavyoitumia inaweza kusababisha madhara makubwa. Teknolojia inaweza kukusababishia ukafukuzwa kazi, inaharibu ndoa nyingi, inaharibu marafiki na vile vile inavuruga malezi ya watoto.

Vile vile inafanyika kuwa kikwazo kwa namna tunavyowasiliana na watu wengine ambavyo hudhaniwa kuwa dharau. Muda mwingi tunaotumia kwenye teknolojia, tunapoamua kuitumia na vile vile ikaathiri hata mahusiano ya ndani kabisa kwenye mahusiano na wapenzi.

Tatizo la teknolojia inawezekana una matumizi mazuri tu kama mjasiriamali, kuangalia barua pepe na hata kuboresha mwonekano wako kwenye mitandao ya kijamii. Inawezekana kutokana na kazi hiyo na muda mwingi unatumia kwenye laptop yako (tarakishi mpakato) na kusababisha kazi nyingine unakuja nazo nyumbani na kushindwa kuwa na muda na mwenzi wako.

Sababu yoyote ile uliyonayo, pale mwenzi wako anapoona unajali sana teknolojia hiyo au simu hiyo kuliko yeye inamaanisha umebeba tatizo mikononi mwako. Na kama uko kwenye ndoa, unajua kitu gani kinaondoa au kupoteza! Hayo ni matatizo ambayo yanahitaji kushungulikiwa ipasavyo,

Je unajuaje kwamba teknolojia imeua au kudhorotesha mahusiano/Ndoa yako? Kuna viashiria vifuatavyo;

1. Una chati au kumtumia jumbe za maneno na mpenzi wako zaidi kuliko kuongea naye.

2. Imekuwa kawaida Unalala na simu yako mkononi au kupitiwa na usingizi huku ukiwa unachati au unaperuzi kwenye mtandao.

3. Unatumia muda mwingi kwenye mtandao kuliko kuwa na mpenzi wako.

4. Ukiwa unaangalia runinga na mpenzi wako, macho yako muda mwingi unayatumia kuangalia simu.

5. Unakuwa na simu yako jikoni na hata mezani wakati wa kula.

6. Kila wakati unaangalia simu yako unaposikia mlio wa meseji au ujumbe wa maneno au mtandao wa kijamii hata kama mpenzi wako anaongea au kukusemesha kitu, unajikuta unapata hamasa ya kuangalia ujumbe huo badala ya kusikiliza.

7. Ukiamka asubuhi kitu cha kwanza ni kuangalia barua pepe, au kwenye mitandao ya kijamii (Instagram, Twitter na Facebook) kabla ya kitu kingine chochote.

Na mambo mengi yanafanyika unahitaji kujua tatizo lako ni nini na unakabiriana nalo vipi.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents