Siasa

Jipya lazuka BOT

Timu iliyoundwa na Raisi dhidi ya kufuatilia pesa zinazodaiwa kuchotwa Benki ya Tanzania BOT kupitia akaunti ya madeni ya nje EPA, ikiwa inaendelea na kazi yake, imekutana na kasheshe jingine jipyaa na safari hii likiwa linadaiwa kuwa baadhi ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 155

Timu iliyoundwa na Raisi dhidi ya kufuatilia pesa zinazodaiwa kuchotwa Benki ya Tanzania BOT kupitia akaunti ya madeni ya nje EPA, ikiwa inaendelea na kazi yake, imekutana na kasheshe jingine jipyaa na safari hii likiwa linadaiwa kuwa baadhi ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 155 zimetumika katika njia isiyo ya halali.

 
Fedha hizo zinadaiwa kutumika kupita mpango wa kampuni ya mgodi wa Meremeta, zikiwa zimelipwa na BOT kwa njia ambayo inaashiria kuna jambo limejificha, ikiwa ni wakati wa uongozi wa aliyekuwa gavana aliyetengulia mbele ya haki Bwana Daudi Balali.

 
Gavana wa sasa wa BOT ni Professa Benno Ndulu, ambaye aliteuliwa kushika wadhifa ili kurekebisha hali ya mambo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa marehemu Dk. Balali, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kupokea ripoti iliyoonyesha kuwa kupitia EPA, BOT ililipa `kifisadi` kiasi cha Sh. Bilioni 133 kwa makampuni mbalimbali nchini.

 
Akilipua bomu hilo mbunge wa Chadema Dk Wilbrod Slaa alisema “Sasa kuna haja ya kufanya uchunguzi mwingine utakaohusiana na suala hili… kuna utata mkubwa kuhusiana na kampuni ya Meremeta ambayo ilidaiwa kuwa ni ya Serikali, lakini taarifa za sasa hazionyeshi kwamba mgodi huo ni wa Serikali,“ akasema Dk. Slaa.

 

 

 

Akasema Dk. Slaa kuwa hadi sasa, hata kamati iliyoundwa na Rais Kikwete tayari imeshasema kuwa katika uchunguzi wake, imebaini kuwa kampuni za Meremeta na Tangold hazimilikiwi na Serikali.

 

 

 

Aidha Dk Slaa alisisitiza kwa kasema kuwa anao ushahidi kuwa kampuni ya Meremeta ilichotewa zaidi ya Shilingi Bilioni 155 kutoka BoT, kwa madai kuwa mgodi huo ni mali ya Serikali.

 
“Maeneo yaliyopigiwa kelele sana na wananchi ni kwenye migodi ya Tangold na Meremeta ambayo imebainika kuwa si mali ya Serikali… tunahitaji sasa uchunguzi ufanyike ili tujue bilioni 155 za walipakodi zimekwenda wapi na kwa nani,“ akasema Dk. Slaa.

 

 

 

Kabla ya kauli hiyo ya sasa ya Dk. Slaa , Mkaguzi na Mdhibiti wa Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Ludovick Utouh, amewahi kunukuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisema kuwa ofisi yake haiitambui kampuni ya Meremeta kama ni mojawapo ya kampuni za umma.

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents