Siasa

JK ateua majaji 7 wanawake

Rais Jakaya Kikwete ameteua majaji 11 wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, huku 7 kati yao wakiwa wanawake. Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu, Bw. Philemon Luhanjo ilisema uteuzi huo umeanza Mei 24 mwaka huu

Na Mwandishi Wa Nipashe

Rais Jakaya Kikwete ameteua majaji 11 wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, huku 7 kati yao wakiwa wanawake. Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu, Bw. Philemon Luhanjo ilisema uteuzi huo umeanza Mei 24 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanawake walioteuliwa kuwa majaji ni Bi. Sophia Wambura, Bi. Crecencia William Makuru, Bi. Zainabu Goronya Muruke na Bi. Upendo Hillary Msuya.

Wengine ni Bi. Atuganile Florida Ngwala, Bi. Rose Aggrey Teemba na Bi. Rehema Kiwanga Mkuye.
Majaji wengine wapya wa Mahakama Kuu ni Bw. Kassim M. Nyangarika, Bw. Gabriel Kamugisa Rwakibarila, Bw. Ibrahim Sayida Mipawa na Bw. Lawrence Kisenge Nziajose Kaduri.

Aidha, Rais Kikwete amemteua Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Bw. Wambali anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bi. Sophia Wambura ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Wambali alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani.


 


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents