Siasa

JK ateuliwa Kamishina wa Tume ya Afrika

Rais Jakaya Kikwete, ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Afrika iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Bw. Anders Fogh Rasmussen ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Na Mwandishi Maalum

 
Rais Jakaya Kikwete, ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Afrika iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Bw. Anders Fogh Rasmussen ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume hiyo.

 

Katika barua yake kwa Rais Kikwete, Bw. Rasmussen alisema Kamisheni hiyo italenga mambo muhimu makuu yanayohusu, “Vijana na ajira“ kwa vile nusu ya raia kusini mwa Jangwa la Sahara ni vijana chini ya miaka 18 ambao hawana mkakati wa uhakika unaohusu ajira.

 

“Kizazi cha vijana kinaweza kutumika katika kuleta maendeleo na ustawi barani Afrika. Malengo mengine ya Kamisheni ni usawa wa kijinsia, mabadiliko ya hali ya hewa, elimu na ukuaji wa uchumi kwani kunahitajika mtazamo mpya wa jinsi ya kuleta maendeleo na kushirikiana ikiwemo misaada na sera sahihi zinazoweza kuchangia katika jitihada za Afrika kwa kutambua michango mbalimbali,“ alisema Bw. Rasmussen katika barua yake kwa Rais Kikwete mapema mwezi huu.

 

Waziri Mkuu wa Denmark alimweleza Rais Kikwete kuwa, amemteua katika Kamisheni hii kwa vile anaamini kuwa upeo wake, uzoefu na uongozi wake mzuri utakuwa na manufaa makubwa katika kuelekeza kazi za Kamisheni hii katika muelekeo mzuri.

 

Kwa upande wake Rais Kikwete amekubali uteuzi huo kwa vile malengo ya Kamisheni yanakwenda sambamba na sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuendeleza vijana na kuongeza ajira ili hatimaye kupunguza umaskini nchini.

 

Kamisheni hii imepanga kuwa na kikao chake cha kwanza katikati ya mwezi wa Aprili, mwaka huu ambapo kikao kitakuwa na kazi ya kupanga mikakati na mbinu za kufikia malengo yake na baadaye mikutano mingine kufuatia katika kipindi cha mwaka mmoja kijacho ambapo mapendekezo na matokeo ya kazi mbalimbali yatatolewa kwa ajili ya utekelezaji.

 

Kamisheni hii pia itaundwa na wawakilishi kutoka taasisi zisizo za kiserikali (NGO’S) na mashirika ya kijamii.

 

Katika vikao vya Kamisheni hii, wadau wakuu wa maendeleo kutoka mashirika ya kimataifa hususan kutoka Afrika, sekta binafsi, wafanyabiashara na wasomi mbalimbali watahusishwa.

 

 

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents