Siasa

JK, hii inatisha!

Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Jakaya Kikwete kutaka waliokatisha masomo mabinti wadogo na kuwaweka kinyumBa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria, limeweka hadharani uozo wa kutisha.

Na Ally Hengo, PST �Kisarawe



Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Jakaya Kikwete kutaka waliokatisha masomo mabinti wadogo na kuwaweka kinyumBa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria, limeweka hadharani uozo wa kutisha.


Miongoni mwa mambo yaliyoanikwa ni kwamba baadhi ya wanaohusika na kuwakatisha masomo watoto ni walimu wao wenyewe.


Kingine kilichobainika ni kwamba zoezi hilo ni gumu mno kutokana na watoto wengi waliokatishiwa masomo kutotoa ushirikiano kwa vyombo vya dola.


Yote hayo yamebainika wakati viongozi wa juu katika mikoa mbalimbali nchini wako `bize` katika kutekeleza agizo hilo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hali hiyo imeelezwa kujitokeza katika mikoa mbalimbali nchini ukiwemo mkoa wa Pwani.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo PST imezinasa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani, Bi. Hanifa Karamagi, ni kwamba hadi sasa, mabinti kibao wameshaachishwa masomo na kubebeshwa mimba wilayani humo huku wengine wakiwa tayari wameshajifungua.


Katika kukabiliana na tatizo hilo, juzi, Bi. Karamagi alitoa agizo la kukamatwa mara moja kwa wazazi kadhaa baada ya kubainika kuwa mabinti kumi waliofaulu la saba na kutakiwa kuanza kidato cha kwanza, wameozeshwa na hivyo kutoripoti mashuleni mwao.


Kutokana na utekelezaji wa agizo hilo la Bi. Karamagi, ndipo ukubwa wa tatizo hilo la kuozeshwa mabinti wadogo ulipobainika zaidi.


Karibu katika kila eneo ambalo askari polisi walimwagwa ili kuwakomboa mabinti hao na kuwarejesha mashuleni, yalikutwa mauzauza ya aina yake.


Afisa mmoja wa polisi aliyeshiriki katika operesheni hiyo ameiambia PST kuwa yeye ameshuhudia mabinti watatu kati ya hao wakiwa na mimba huku wawili wakiwa na vichanga.


Mbaya zaidi, ikaelezwa na afisa huyo kuwa hakuna binti aliyekuwa tayari kumtaja aliyempa mimba.


Juzi jioni, katika tukio `latest` kabisa kuhusiana na kuozeshwa kwa bei poa kwa mabinti wanaokatishwa masomo Kisarawe, binti mmoja aliibuliwa kule Tabata Matumbi Jijini Dar akiwa tayari ana kichanga cha mwezi mmoja na nusu.


Ufuatiliaji wa binti huyo ulikuja baadaya Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mzenga, Bw. Ridhiki Mlembe kupasua siri hiyo kwa Mkuu wa wilaya kwamba binti mmoja mdogo aliyefaulu, ameozeshwa Jijini Dar.


Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa wilaya alicharuka na kumwamuru kamanda wa polisi wa wilaya ya Kisarawe, Afisa elimu wa wilaya pamoja na mtendaji huyo haraka kumkamata mzazi huyo siku hiyo hiyo bila kusubiri ili waende naye Dar es salaam na kumtia mbaroni huyo anayeishi na binti huyo.


Alitaka watapokamatwa, wafikishwe mbele yake na yeye mwenyewe ndiye atakayechukua jukumu la ulalamikaji kwa wote waliohusika kuhujumu elimu ya binti huyo, ili watapofikishwa kwenye vyombo vya sheria, liwe fundisho kwa wazazi wanaondekeza tabia hiyo iliyoota mizizi.


Hata hivyo walipomfuatilia binti huyo Jijini walikuta tayari ana kichanga chake na wala hayuko tayari kuwapa ushirikiano.


Souce: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents