Michezo

JKT Ruvu: Kubaki ligi kuu ni kudra za Mungu

Jkt Ruvu baada ya kukubali kipigo hapo jana dhidi ya Toto Africans ya Mwanza, msemaji wa klabu hiyo Konstantin Masanja amekiri kuwepo na hati hati ya kushuka daraja.

“Tumepoteza mchezo wa jana timu ya Jkt Ruvu huku wachezaji wote kutokupata majeruhi na kila mchezaji anaonekana kuwa na hari nzuri, kwanza huu ni mchezo, lolote linaweza kutokea katka kipindi cha dakika 90, Jkt Ruvu tulicheza vizuri tukaanza kuwafunga goli ndani ya dakika moja ya kipindi cha kwanza”.

“Lakini wenzetu waliweza kuyarudisha magoli yote mawili katika kipindi cha kwanza, na mpira wa jana sisi Jkt Ruvu ulikuwa muhimu sana katika kuweka hai matumaini yetu ya kubaki katika ligi kuu ya Vodacom lakini wenzetu Toto Africa nao kwa upande wao walijipanga vizuri katika kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa jana”..

“Kwa takwimu za uwiano wa alama, ni kweli Jkt Ruvu tunaelekea kushuka Daraja, lakini uhakika wa kushuka daraja bado kwani ligi kuu ya Vodacom bado hajaisha, bado tuna mechi mbilihatakama tutashuka daraja bado tamko rasmi la kwamba timu ngapi zitashuka daraja bado kwani zinaitajika timu tatu za kushuka daraja bado tupo katikaligi kuu ya Vodacom na tunaendelea na mashindano”.

Jkt Ruvu ipo nafasi ya 16, inaburuza Mkia wakiwa na alama 23 wamecheza michezo 28, na nafasi ya 15 ni klabu ya maji maji wakia na alama 29 wamecheza michezo 28, nafasi ya 14 ni Toto Africa wamecheza michezo 27 wana alama 29 na nafasi ya 13 ni Ndanda wenye alama 30 wakiwa wamecheza michezo 28, na nafasi ya 12 ni klabu ya Mbao Fc wenye alama 30 sawa na Ndanda.

Timu hiyo inakibarua kizito mchezo ujao dhidi ya Majimaji katika uwanja wao wa nyumbani wa Mkwa Mkoani Tanga na kisha kwenda Mtwara kabla ya kumalizia safari yao kwa wana kuchele ya klabu ya Ndanda Fc.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents