Joe Biden athibitishwa mshindi tena, baada ya kura kuhesabiwa upya Georgia

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amethibitishwa kushinda uchaguzi Georgia baada ya kura kuhesabiwa tena, huku juhudi za kisheria za washirika wa Donald Trump kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo matatu zikitupiliwa mbali.

Biden wa Democratic alimshinda mpinzani wake Trump wa Republican katika jimbo la Georgia kwa kura 12,284, kwa mujibu wa ukaguzi unaohitajika na sheria ya mamlaka ya majimbo.

Bwana Biden alisema Trump alijua kwamba atashindwa na ameonesha “kutowajibika” kwa kukataa kukubali matokeo.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Democratic anajiandaa kuingia madarakani mwezi Januari kama rais wa 46 wa Marekani.

Ushindi wa Bwana Biden unaonesha alipigiwa kura zaidi ya milioni 5.9. Katika mfumo wa uchaguzi kupitia wajumbe maalum, ambao unaamua ni nani atakuwa rais, Biden alipata kura 306 dhidi ya 232 – zaidi ya 270 alizohitaji kushinda.

Kufikia sasa Bwana Trump hajakubali kushindwa na ametoa madai ya udanganyifu katika mchakato wa uchaguzi bila kutoa ushahidi wowote.

Kufikia sasa Bwana Trump hajakubali kushindwa na ametoa madai ya udanganyifu katika mchakato wa uchaguzi bila kutoa ushahidi wowote.

Ni nini kilifanyika Georgia?

Siku ya Alhamisi, Waziri wa mambo ya nje wa Georgia Brad Raffensperger, alisema ukaguzi wa mkono wa kura haujabadilisha ushindi wa Bwana Biden katika jimbo hilo.

“Ukaguzi wa kwanza wa kihistoria wa kura katika jimbo zima la Georgia umethibitisha tena kuwa mfumo mpya wa upigaji kura na kuhesabu kura na uhasahihi wa matokeo” Bw. Raffensberger, wa Republican, alisema katika taarifa.

“Hii ni sifa inayoashiria bidii ya wafanyakazi wetu wa kaunti na maafisa wa uchaguzi wa mitaa ambao walifanya shughuli ya kuhesabu tena kura kwa haraka na kutumia muda mfupi.”

Ushindi wa Democrats katika jimbo la Georgia ni wa kwanza katika uchaguzi wa urais tangu Bill Clinton alipochaguliwa mwaka 1992.

Matokeo baada ya kuhesabiwa tena

Matokeo baada ya kuhesabiwa tena

Wakati wa kurudiwa hesabu ya kura ilibainika kuwa kiwango cha makes hakikuwa kikubwa kuliko asilimia 0.73 katika kaunti yoyote na kwamba ushindi wa Bw. Biden dhidi ya Bw.Trump ulisalia chini ya asilimia 0.5%. Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kuidhinishwa rasmi waakt wowote.

Mashauri wa kisheria wa kampeni ya Trump, Jenna Ellis amesema matokeo ya ukaguzi yalifanyika “kama ilivyotarajiwa”, alisema bila kutoa ushahidi wowote kwama jimbo hilo lilirudia kuhesabu kura ambazo si halali.

Lakini Gabriel Sterling, Mrepublican ambaye anahudumu kama meneja msimamizi wa utekelezaji wa mfumo wa upigaji kura, ameambia CNN siku ya Alhamisi: “Moja ya malalamiko makubwa ya mashine hizi kwa njia fulani zinageuza kura au kubadilisha kura na kadhalika. Dosari hizo hazikujitokeza hapa Georgia. Tumethibitisha hilo.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW