Soka saa 24!

Joe Cole atangaza kustaafu soka

Joe Cole, aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Uingereza, ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 37.

Cole, ambaye amewahi kuzitumikia timu mbalimbali zikiwemo West Ham, Chelsea,  Liverpool, Lille, Aston Villa, Coventry City ametangaza kustaafu leo Novemba 13, akielezea kazi yake ya mpira aliyokuwa akiifanya kwa nuda wa miaka 20 kama  ‘a dream come true.’

 

Kustaafu kwake kumekuja mara baada ya kuitumikia timu ya  Tampa Bay Rowdies kwa muda wa miaka miwili na nusu imayoshiriki  ligi ya United Soccer League huko nchini  Marekani.

“After 20 years of living my dream, the time has come for me to hang up my boots…” aliandika hivyo katika kurasa zake za Instagram.

Joe Cole aliwahi kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Mawili ya FA Cups na kufika hatua ya fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa UEFA mwaka 2006.

 

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW