Burudani

Joh Makini akwepa kuizungumzia ishu hii kuhusu Fid Q

Msanii wa muziki wa hip hop wa Kundi la Weusi, Joh Makini amesita kuizungumzia ishu ya ushindani kati yake ya rapa kutoka Mwanza Fareed Kubanda ‘Fid Q’.

Mashabiki katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakiwashindanisha wawili hao kutokana na uwezo wao wakuandika mistari nakuchana hali ambayo ilitengeneza taswira ya kwamba huwenda hawaelewani kitu ambacho kiliwekwa sawa na wawili hao hivi karibuni.

Mtangazaji JJ wa Jembe Fm ya Mwanza, alipiga stori na Joh Makini na kumuuliza kama ushindani wake na Fid Q umekwisha baada ya hivi karibuni wawili hao kuonekana hawana tatizo.

“Actually ni vitu ambavyo sipendi kuvipa nafasi kwenye muziki wangu kwa sababu siamini katika hivyo vitu kwenye muziki wangu toka nimeanza mpaka nimefika hapa,” alijibu Joh Makini.

Rapa Fid Q hivi karibuni alidai hakuwa na ushindani na rapa huyo wa Kundi la Weusi ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Yakulevya’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents