Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Joh Makini ataja timu tano zitakazofanya vizuri Kombe la Dunia 2018 (+video)

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Joh Makini ametaja timu tano ambazo anaona zitafanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Rapper huyo kutoka kundi Weusi ametaja timu hizo kuwa ni German, Brazil, France, Spain na Belgium

“Kusema kweli mchuano ni mgumu kwa sababu kuna timu kama tano ambazo ni hevy, let say German, Brazil, France, Spain na Belgium ambayo watu wengi haitazami lakini mimi naitazama kwa jicho la tatu, naona kama inaweza kufanya makubwa,” Joh Makini ameiambia Bongo5.

Katika hatua nyingine Joh Makini amesema mchezaji anayemtazama zaidi katika michuano hiyo ni Christian Ronaldo kutoka Ureno.

“Mimi ni shabiki mkubwa wa Ronaldo, imetokea tu, anani-inspire kwa jinsi ambavyo jamaa anaonekana anafanya mazoezi na anajituma. Ni mtu ambaye anadhihirisha unaweza kuwa na kipaji usiwe bora,” amesema Joh Makini.

Michuano ya Kombe la Dunia ambayo inajumuisha timu za mataifa 32 inaanza leo June 14, 2018 nchini Urusi. Katika mchezo wa ufunguzi utakutanisha timu mwenyeji ambayo atajitupa dimbani kuikabili Saudia Arabia.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW