Soka saa 24!

Joh Makini kuiendesha The Countdown ya Choice FM wiki hii

Mweusi Joh Makini wiki hii atakiendesha kipindi cha The Countdown kinachorushwa na kituo cha radio cha Choice FM 102.5, Dar es Salaam.

Joh-makini

The Countdown huruka kuanzia saa tisa mchana hadi za 11 jioni. Ni kipindi cha kila wiki ambacho huwa na mkusanyiko wa nyimbo 20 bora zilizochaguliwa kwa mapenzi yake mtu maarufu kwenye maeneo mbalimbali husasan katika tasnia ya burudani.

The Countdown hucheza nyimbo 20 zilizochaguliwa na mtangazaji wa wiki husika. Nyimbo hizo huzichagua mwenyewe kulingana na muziki anaopenda kuusikiliza kila siku. Hizo huwa ni nyimbo zinazotafsiri wajihi wao pamoja na nyimbo ambazo ziliwasaidia katika vipindi mbalimbali vya maisha yao.

Wiki hii hitmaker huyo wa ngoma kibao zikiwemo, Hao, Copy My Motion, Byebye, Kilimanjaro, Manuva na zingine atawapa wasikilizaji wa The Countdown ladha ya muziki anaoupenda. Msikilizaji atapata fursa ya kusikia Joh ni mtu wa aina gani kwa kumchezea nyimbo zake 20 bora. The Countdown hutayarishwa na Maribeth Vuhahulla ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds TV.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW