Burudani

Joh Makini na Davido hawajaamua nani atamiliki wimbo watakaofanya

Joh Makini amesema bado yupo kwenye mazungumzo na Davido ili kujua nani atakuwa mmiliki wa wimbo watakaofanya au kama utakuwa unamilikiwa na wote.

joh davido

Rapper huyo amesema ikifika wakati ataweka wazi kila kinachoendelea kwenye kazi hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

“Ni mapema zaidi kujadili wimbo utakuwa ni wa kwake au wa kwangu hadi kila kitu kitakapokamilika ramsi. Kwa sababu bado tupo kwenye mazungumzo ya kujadili ni wa kwake au wa kwangu au wa wote,” Joh Makini aliambia XXL ya Clouds FM.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents